Highlights

Polisi Marsabit Central wanachunguza kisa cha wizi wa boda boda, Majengo

Na Caroline Waforo

Polisi katika kaunti ndogo ya Marsabit Central wanachunguza kisa cha wizi wa boda boda usiku wa jana Jumapili katika eneo la Majengo.

Kulingana na OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago, mhudumu mmoja wa boda boda aliripoti kutishiwa kwa kisu na wateja wawili aliokuwa amewabeba kabla ya kuibiwa kwa pikipiki hiyo walipofika mwisho wa safari.

Tukio hili linajiri baada ya kisa kingine cha wizi wa boda boda kuripotiwa mwishoni mwa mwezi Aprili katika eneo la Milima Tatu.

Hata hivyo, vipande vyote vya boda boda hiyo vilipatikana, baada ya washukiwa wawili kukamatwa na kusaidia maafisa wa polisi katika uchunguzi.

OCPD Gachago amewahimiza wahudumu wa boda boda kuwa makini na kuchukua tahadhari hasa nyakati za usiku na kuepuka kubeba abiria zaidi ya mmoja ili kupunguza hatari ya kushambuliwa.

Post Comment