Highlights

Wazazi Marsabit wahimizwa kurejesha watoto shuleni kwa muhula wa pili ulioanza wiki iliyopita

Na JB Nateleng

Wazazi katika jamii za wafugaji, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanawarejesha watoto wao shuleni kwa muhula wa pili ulioanza wiki iliyopita.

Wito huo umetolewa na Chifu wa eneo la Baala, Korr katika eneo bunge la Laisamis, Job Hirkena Eithimole ambaye amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha watoto wanarudi shuleni bila kuchelewa.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Hirkena amewahimiza wazazi kujituma na pale inapobidi kuuza sehemu ya mifugo yao ambayo kwa sasa iko katika hali nzuri kufuatia mvua iliyonyesha katika eneo hilo akisema hatua hii itasaidia kupata fedha za kulipia karo na mahitaji mengine ya shule kwa wanafunzi.

Kauli yake inajiri wakati ambapo wanafunzi wamerejea shuleni kwa muhula wa pili mnamo tarehe 27 Aprili 2026, unaotarajiwa kumalizika tarehe 31 Julai 2026.

Kulingana na kalenda ya masomo wanafunzi watapata likizo fupi kuanzia tarehe 24 Juni hadi 28 Juni 2026.

Huku likizo ya agosti ikianza tarehe 3 Agosti 2026 hadi 21 Agosti 2026.

Post Comment