Highlights

Mwanaume mmoja ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumnajisi msichana wa miaka 11, Moyale

Mahakama ya Moyale imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha maisha gerezani kwa kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 11 katika lokesheni ya Dabel kaunti ndogo ya Moyale.

Ibrahim Hassan alipatikana na hatia ya kumnajisi msichana huyo mnamo tarehe 7 mwezi Februari mwaka 2025.

Hukumu hiyo ilitolewa jana Ijumaa na Hakimu Mkaazi wa mahakama hiyo ya Moyale Kombe Larry baada ya upande wa mashkata kuwasilisha mashahidi wanne akiwemo mwathiriwa.

Kulingana na ripoti za mahakama mwaathiriwa alieleza mahakama kuwa usiku wa mkasa alienda kulala pamoja na ndugu zake na alipoamka mida ya saa kumi na mmoja na nusu asubuhi alipa yuko uchi huku mhukumiwa akilala kando yake akiwa uchi.

Mhukumiwa ana siku 14 kukata rufaa.

Post Comment