Highlights

Mwalimu afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi Kargi.

Na Mwandishi wetu

Mwalimu aliyekamatwa wiki jana kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa miaka 14 katika kaunti ndogo ya Loiyangalani, amefikishwa katika mahakama ya Marsabit Leo Jumatatu.

Mshukiwa Dennis Kipkoech Chepkwony amefikishwa mbele ya hakimu Edward Oboge ambapo pia ameshtakiwa kwa kosa la kumshika visivyo mwanafunzi huyo.

Mshukiwa anadaiwa kutekeleza kosa hilo kati ya tarehe 5 hadi 18 mwezi Aprili mwaka 2026.

Hakimu ameagiza idara ya probesheni kuwasilisha ripoti kutathmini iwapo mshukiwa anaweza kuachiliwa kwa bondi au la.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 8 mwezi Juni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment