Loading Now

Highlights

Mvua zaanza mapema Marsabit huku hali ya ukame ikiendelea kufuatiliwa.

Na Samuel Kosgei

Mvua za msimu wa masika zimeanza kunyesha mapema kuliko kawaida katika baadhi ya maeneo ya kaunti ya Marsabit, hali inayorejesha matumaini kwa wakazi wanaokabiliwa na athari za ukame.

Kulingana na ripoti ya hali ya ukame ya mwezi uliopita kutoka kwa mamlaka ya kukabiliana na ukame NDMA, mvua zimeanza takribani mwezi mmoja mapema na zimeshuhudiwa katika maeneo ya Saku, North Horr, Moyale na sehemu za Laisamis.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa wakazi wameanza kutegemea zaidi vyanzo vya maji ya wazi pamoja na maji yanayokusanywa kutoka mapaa ya nyumba kufuatia kuanza kwa mvua hizo.

Kwa upande wa mifugo, hali ya miili ya mifugo mingi imeelezwa kuwa ya wastani na iko katika kiwango cha kawaida. Hata hivyo, uzalishaji wa maziwa kwa kila kaya unasalia chini ya kiwango cha kawaida, huku kaya zikizalisha wastani wa lita 1.2 pekee kwa siku.

Wakati huo huo, wakulima bado hawajaanza kupanda mazao mashambani, huku wengi wao wakiendelea na maandalizi ya mashamba na upanzi wa mapema.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa visa vya vifo vya ngamia vinavyohusishwa na ugonjwa wa Acute Camel Death Syndrome viliripotiwa katika mwezi uliopita.

Post Comment