Highlights

Kesi ya uchafuzi wa mazingira Kargi na Maikona yapangiwa kutajwa Juni 11.

Na Samuel Kosgei

Mahakama ya Mazingira na Ardhi mjini Isiolo imeipa jamii ya maeneo ya Kargi na Maikona siku 21 kuwasilisha rasmi kesi ya uchafuzi wa mazingira dhidi ya kampuni ya BP kupitia wizara ya mashauri ya kigeni au ubalozi husika.

Hatua hiyo imejiri wakati mahakama hiyo iliposikiliza kesi kuhusu madai ya uchafuzi wa mazingira unaodaiwa kusababishwa na taka hatari zilizosalia baada ya shughuli za zamani za utafutaji wa mafuta kaskazini mwa Kenya.

Kesi hiyo inahusisha madai kuwa shughuli za zamani za kampuni ya Amoco Corporation, ambazo baadaye zilichukuliwa na BP, zilichangia uharibifu wa muda mrefu wa mazingira katika maeneo ya Kargi na Maikona.

Walalamishi wanadai kuwa taka hizo zimekuwa tishio kwa afya ya wakazi pamoja na kuharibu mazingira ya maeneo hayo kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, taasisi ya Katiba Institute imeruhusiwa kujiunga katika kesi hiyo kama mdau mwenye maslahi maalum na inatarajiwa kuwasilisha hoja zake mahakamani.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 11 Juni mwaka 2026.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment