Highlights

Mwalimu akamatwa kwa tuhuma za kumnajisi na kumpachika mimba mwanafunzi wake wa gredi saba, Kargi

Na Caroline Waforo

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Mission of Hope International iliyoko Kargi kaunti ndogo ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit amekamatwa kwa tuhuma za kumnajisi na kumpachika mimba mwananfunzi wake wa gredi ya saba aliye na umri wa miaka 14.

Akithibitisha kisa hicho OCPD wa Loiyangalani Nicholas Mutua amesema kuwa uchunguzi unaashiria kuwa mwaathiriwa ana ujauzito wa miezi mitatu.

Aidha, Mutua amesema kuwa madai yameibuka kuwa si mara ya kwanza kwa mshukiwa kuhusishwa na visa vya aina hiyo, huku akidaiwa kuwapachika mimba wanafunzi wengine wanne katika eneo la Kargi.

Amesema kuwa mwalimu huyo tayari amekamatwa huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini ukweli wa madai hayo na hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa

OCPD Mutua amesema kuwa vipimo vya msimbojeni DNA vitafanyika kusaidia katika uchunguzi huo.

Aidha amewataka wananchi kushirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama kwa kuripoti visa vya dhuluma dhidi ya watoto mapema ili hatua zichukuliwe haraka.

Vilevile OCPD Mutua ametoa onyo kali kwa wanaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto akisema watachukuliwa hatua kali za kisheri.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Muyanzi

I would suggest that before reporting something or any case to the social media…get to the ground and know what the real information is.Reporting what is not true is even against the legal policies and against the law.
Do your research properly because we are the ones on the ground and also the first bearers of the story and case and not you all.
Kind Regards

Post Comment