Familia ni nguzo ya malezi na utambuzi wa wito wa maisha asema Padri Joseph Ng’ang’a.
NA JB Nateleng
Familia imetajwa kuwa nguzo muhimu katika kuwalea watoto na kuwasaidia kutambua wito sahihi wa maisha unaochangia ustawi wa kanisa.
Haya yamesemwa na Padri Joseph Ng’ang’a wa shirika la Comboni Missionaries of the Heart of Jesus, anayesimamia masuala ya miito.
Akizungumza na Radio Jangwani, Padri Joseph amesema ni wajibu wa wazazi kuwalea watoto kwa misingi ya kanuni za kanisa na maagizo ya Mungu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya maisha, ikiwemo kumtumikia Mungu kama kasisi, mtawa au mhudumu wa kanisa.
Aidha, Padri Joseph amesema mila na tamaduni za baadhi ya jamii za Afrika zimechangia kupungua kwa idadi ya vijana wanaojiunga na mashirika ya kimishonari. Hata hivyo, amewahimiza wazazi na vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kanisa na kutembelea parokia ili kusaidiwa kutambua wito wao.



Post Comment