Caritas na serikali ya marsabit wahimiza ujumuishwaji wa watu wanaoishi na ulemavu
Na Joy Akinyi & Sabalua Moses
Shirika lisilo la kiserikali la CARITAS kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Marsabit limeandaa hafla iliyowaleta pamoja watu wanaoishi na ulemavu pamoja na washikadau mbalimbali kuadhimisha siku ya kimataifa ya kujumuisha watu wanaoishi na ulemavu katika nyanja zote za jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Kamishna wa Marsabit Central, Mathew Wambugu, amesema serikali kuu imehakikisha kuwa watu wanaoishi na ulemavu wanapata huduma bora kupitia serikali ya kitaifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu katika Idara ya Huduma za Jamii, Galgallo Okotu, amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha watu wanaoishi na ulemavu wanapata huduma kwa urahisi na kwa usawa, ikiwemo katika sekta za afya, elimu na ajira.
Naye Peter Okello, afisa mkuu anayesimamia programu katika shirika la CARITAS, amesema kuna changamoto ya ukosefu wa vifaa vya usaidizi vinavyowawezesha watu wanaoishi na ulemavu kupata huduma kwa urahisi.
Aidha, mchanganuzi wa masuala ya huduma za jamii, Salome Kimata, amesema kuna haja ya kuwajumuisha watu wanaoishi na ulemavu katika shughuli za kawaida za kijamii pamoja na sekta mbalimbali.



Post Comment