Baba akamatwa kwa tuhuma za kujaribu kumnajisi mwanawe wa miaka 12, Loglogo
Na Caroline Waforo
Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za kujaribu kumnajisi mwanawe wa miaka 12 katika kijiji cha Lbarok Lokesheni ya Loglogo, kaunti ndogo ya Marsabit Kusini.
Kulingana na OCPD wa Marsabit Kusini Mohammed Mwakio, kisa hicho kiliripotiwa siku ya Jumapili na mama mzazi wa mwathiriwa ambaye alidai kuwa tukio hilo lilitendeka nyumbani kwao.
OCPD Mwakio ameseme kuwa mwanaume huyo anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku ya hapo kesho Alhamisi huku akiwahakikishia wakaazi eneo hilo kuwa uchunguzi wa kina unaendelea na haki itatendeka.
OCPD Mwakio ametoa onyo dhidi ya dhulma za kingono akisisitiza kuwa washukiwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile ameitaka jamii kwa pamoja kushirikiana na idara za usalama ili kukomesha visa hivi vya unajisi vinavyozidi kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.
Aidha Mwakio amesema kuwa bado wanaendelea kumsaka mshukiwa wa ulawiti katika eneo la LogLogo. Mshukiwa huyo wa miaka 16 anatuhumiwa kumlawiti mtoto wa miaka 10 walipokuwa malishoni majuma kadhaa yaliyopita.



Post Comment