Loading Now

Highlights

Wakaazi Marsabit Central wahimizwa kutafuta njia mbadala za mapato ili kupunguza utegemezi mkubwa wa misaada

Wakaazi Marsabit Central wamehimizwa kuangazia njia mbadala za kujitafutia mapato ili kupunguza utegemezi mkubwa wa misaada kutoka kwa serikali na wahisani.

Ni wito ambao umetolewa na Mwakilishi wadi wa Marsabit Central Jack Elisha ambaye amewataka wananchi kuwekeza katika shughuli mbadala za kiuchumi kando na ufugaji ili kuimarisha maisha yao na kukomesha hulka ya kutegemea misaada.

Na huku wananchi wakiendelea kukabiliana na uhaba wa chakula na maji kutokana na athari za ukame, Elisha ametoa wito kwa serikali kuu kuongeza mgao wa misaada ya chakula haswa kwa makundi maalum katika jamii.

Post Comment