Highlights

Muungano wa KUCO wakosoa serikali ya Marsabit kwa kushindwa kutatua malalamishi ya muda mrefu

NA Caroline Waforo

Muungano wa Maafisa wa Kliniki nchini KUCO umekosoa serikali ya kaunti ya Marsabit kwa kushindwa kutatua malalamishi ya muda mrefu ya maafisa wake wa kliniki.

Katibu mkuu wa muungano huo George Gibore amesema kuwa serikali ya kaunti ya Marsabit imeshindwa kutekeleza makubaliano ya kurejea kazini huku akisisitiza kuwa lazima matakwa yote yashughulikiwa kabla ya maafisa hao kurejea kazini.

Kaunti nyingine iliyo kwenye mgomo ni kaunti ya Nairobi.

Muungano wa KUCO ulisitisha mgomo wa kitaifa tarehe 28 Januari baada ya kuafikia makubaliano na serikali 44 za kaunti huku kaunti za Marsabit, Nairobi na kaunti ya Baringo zikikosa kutia saini makubaliano hayo.

Maafisa wa kaunti ya Baringo tayari wamerejea kazini baada ya kuafikia makubalino na serikali ya kaunti.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment