Highlights

Polisi warejesha mifugo 204 iliyoibiwa Gudas huku ngamia saba walioibiwa Shurr wakipatikana.

Na Samuel Kosgei

Idara ya usalama katika Kaunti ya Marsabit imesema imefanikiwa kurejesha mbuzi 204 kati ya mbuzi 1,110 walioibwa katika shambulizi la wizi wa mifugo lililotokea eneo la Gudas, Loglogo, katika eneobunge la Laisamis wiki iliyopita.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, ameiambia Radio Jangwani kuwa maafisa wa usalama, kwa ushirikiano na wadau wengine, wanaendelea na juhudi za kuwasaka wahusika na kurejesha mifugo iliyosalia. Amesema mifugo mingine iliyoibwa ni ng’ombe wanane, ndama wanane na punda saba.

Wakati huo huo, Kamanda Kimaiyo amesema ngamia saba kati ya wanane walioibwa katika eneo la Shurr, Wadi ya Turbi, wamepatikana na watakabidhiwa wamiliki wao.

Post Comment