Mama ajifungua watoto watano Marsabit.
Na JB Nateleng
Mama mwenye umri wa miaka 20 kutoka eneo la Olturot, Loiyangalani, amejifungua watoto watano katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit.
Akithibitisha tukio hilo, mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Kusu Abduba, amesema mama huyo alijifungua watoto hao leo, wavulana watatu na wasichana wawili.
Abduba amesema watoto hao wanaendelea kupokea huduma maalum hospitalini na wamewekwa kwenye mashine za mashine ya kuwatunza watoto njiti kutokana na kuzaliwa na uzito wa chini ya kiwango kinachohitajika.
Ameongeza kuwa hali ya mama pamoja na watoto inaendelea kufuatiliwa kwa karibu na wahudumu wa afya.



Post Comment