Loading Now

Highlights

Ongezeko la mafua na homa miongoni mwa jamii lawatia wasiwasi wakazi wa Loiyangalani.

NA Samuel Kosgei

MWAKILISHI wa wadi ya Loiyangalani, Musa Emojo, ameihimiza idara ya afya katika kaunti ya Marsabit kufanya uchunguzi wa haraka kubaini chanzo cha ongezeko la mafua miongoni mwa wakazi wa Loiyangalani na maeneo ya karibu.

Akizungumza na Shajara, Emojo amesema idadi kubwa ya wakazi, hususan watoto, wanakumbwa na kikohozi kikali na mafua kwa wakati mmoja, hali anayoeleza kuwa si ya kawaida.

Ameitaka idara ya afya katika eneobunge la Laisamis kuchukua sampuli kutoka kwa waathiriwa ili kubaini iwapo ni homa ya kawaida au maambukizi ya ugonjwa usiojulikana.

Kuhusu vituo vya afya vilivyojengwa lakini havitumiki, Emojo amesema mchakato wa kununua vifaa muhimu vya matibabu unaendelea pamoja na ajira ya wauguzi wapya.

Ameongeza kuwa tayari amefanya mazungumzo na idara husika, akibainisha kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni ukosefu wa fedha za kutosha, kulingana na majibu aliyopewa.

Post Comment