Loading Now

Highlights

Wakazi wa Marsabit Watakiwa kupnda miti na Kulinda Misitu Wakati huu wa Mvua

Na JB Nateleng

Wakazi wa Marsabit wamehimizwa kuchukua jukumu la kulinda na kutunza misitu, hasa katika msimu huu wa mvua, ili kupunguza hatari ya mafuriko na kuhifadhi mazingira.

Afisa Mkuu Msimamizi wa Idara ya Huduma za Misitu nchini (KFS) katika kaunti ya Marsabit, Kennedy Muthuri, amesema juhudi za pamoja katika upanzi na utunzaji wa miti ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na kituo hiki akiwa ofisini mwake, Muthuri amesema hali ya misitu katika kaunti ya Marsabit inaendelea kuimarika, huku akibainisha kuwa hatua ya wafugaji kuondoa mifugo ndani ya misitu imechangia pakubwa katika uhifadhi wake.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wakazi na Idara ya Misitu ili kufanikisha juhudi za upanzi wa miti na uhifadhi wa mazingira jimboni.

Post Comment