Loading Now

Highlights

Wafugaji Laisamis wahimizwa kulisha mifugo kwa amani msimu huu wa kiangazi

Wafugaji katika eneo la Laisamis kaunti ya Marsabit wamehimizwa kulisha mifugo yao kwa amani msimu huu wa ukame.

Akizungumza na Shajara naibu kamishna wa Laisamis Kepha Maribe amesema kuwa idara ya usalama imeimarisha mikakati ya kiusalama ili kuzuia mizozo ya maeneo ya malisho kutokana na uhaba wa maji na lishe.

Vilevile amedokeza kuwa serikali kuu imeendelea kutoa msaada wa chakula katika eneo hilo.

Post Comment