Mwanaume mmoja ahukumiwa kifungo cha maisha gereza kwa kumlawiti mvulana wa miaka 6, Marsabit Central
Mahakama ya Marsabit imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha maisha gerezani kwa kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa umri wa miaka 6, katika eneo la Township kaunti ndogo ya Marsabit Central.
Mhukumiwa Roba Tura amepatikana na hatia ya kumlawiti mtoto huyo mnamo tarehe 8 mwezi April 2025.
Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa amesema kuwa ushahidi uliyowasilishwa mahakamani umebaini kuwa Roba alimlawiti mvulana huyo ambaye kipindi hicho alikuwa mtoto wa kurandaranda mitaani.
Mwanaume huyo anasiku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.



Post Comment