Loading Now

Highlights

Gavana Mohamud Ali aungana na magavana wenzake kukashifu maseneta kwa madai ya hongo

NA Caroline Waforo

Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali ameungana na magavana wenzake kukashifu kamati ya uhasibu ya bunge la seneti kwa madai ya kuitishwa hongo na kuhangaishwa na kamati hiyo.

Akizungumza katika kongamano la siku nne la baraza la magavana katika kaunti ya Kilifi, Gavana Ali pia amepuuzilia mbali madai ya kamati hiyo ya uhasibu kuwa baraza la magavana limeibua madai ya hongo ili kukwepa uwajibikaji.

Baraza hilo la magavana sasa limetishia kuwasilisha majina ya maseneta wanaoitisha hongo katika vikao vya kamati ya seneti ya uhasibu na kuhujumu utendakazi wa magavana.

Mwenyekiti wa baraza la magavana Ahmed Abdullahi amemuandikia barua spika wa seneti Amason Kingi kuandaa kikao cha dharura na magavana la sivyo hawatafika mbele ya seneti kujibu maswali.

Nao wanakamati wa kamati hiyo ya uhasibu wakiongozwa na seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ wamepuuzilia mbali madai hayo wakiwataka magavana kuwasilisha ushahidi.

Post Comment