Loading Now

Highlights

Wito umetolewa kwa wazazi kuwalinda wasichana wakati wa likizo.

Na Sabalua Moses

Wito umetolewa kwa wazazi kuwa waangalifu na watoto wao wanapoanza likizo fupi. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la Wong`an women Initiative, Teresalba Sintiyan.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Sintiyan amesema kuwa mara nyingi wakati wa likizo fupi, baadhi ya jamii za wafugaji hutumia fursa hiyo kuwaoza wasichana au kuwafanyia ukeketaji.

Hata hivyo, amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa ipasavyo, hasa watoto wa kike.

Aidha, Sintiyan amewataka watoto kuwa waangalifu na kuepuka kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya au kujiunga na makundi mabaya yanayoweza kuwapotosha wakati wa likizo.

Post Comment