Loading Now

Highlights

Wanaskauti Marsabit wafanya uchaguzi

Na JB Nateleng

Wanachama wa skauti katika kaunti ya Marsabit wamechagua viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika uchaguzi huo, Fatuma Kurungu Laigwanani alichaguliwa kuwa mwenyekiti, huku John Pope Wambisa akiteuliwa kuwa Kamishna wa Skauti kaunti ya Marsabit.

Aidha, Yustine Esekon Lokorikau alichaguliwa kuwa Naibu Kamishna anayesimamia mafunzo ya wanachama kuhusu sheria na taratibu za skauti.

Michael Mwaselwa Mackenzie naye aliteuliwa kuwa Naibu Kamishna anayehusika na uratibu wa programu za vijana, huku Teresia Subukia Lenapir akichaguliwa kuwa mwakilishi wa vijana wa skauti katika kaunti ya Marsabit

Uchaguzi huo unaashiria mwanzo mpya kwa chama cha skauti Marsabit, ukiwa na matumaini ya kuboresha utendaji na kuimarisha shughuli zake.

Wakati huo huo, vijana katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kujiunga na chama cha skauti ili kujifunza maadili, kupata ujuzi muhimu na kujenga mustakabali wao.

Post Comment