Wakaazi Marsabit wapendekza nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa akiba NPR
NA Caroline Waforo
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wamependekeza serikali kuboresha maslahi ya maafisa wa akiba NPR kwa kuwapa nyongeza ya mishahara.
Wakizungumza katika kikao cha ushirikishwaji wa umma kuhusu rasimu ya sera ya utendakazi wa maafisa wa NPR, wananchi wamesema kuwa maafisa hao wanaolipwa shilingi 5,000 kwa mwezi wanatekeleza majukumu muhimu ya kulinda maisha na mali, ila hawapati motisha wa kutosha.
Baadhi ya walitoa hoja zao katika kikao hicho kilichoandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki leo Alhamisi, pia wameitaka serikali kuhakikisha kuwa maafisa hao wanalipwa kwa wakati.
Vilevile wananchi wamependekeza maafisa wa NPR kubadilishiwa sare ingawa hoja hiyo imepingwa na msimamiziwa maafisa hao Shukri Huqa.
Sera hiyo pia imepongezwa na mwakilishi wadi wa Karare Joseph Leruk na yule wa Marsabit Central Jack Elisha huku pia wakiitaka serikali kuongoeza idadi ya maafisa wa NPR humu jimboni Marsabit.
Mkrugenzi wa mafunzo na utafiti katika Huduma ya Polisi ya taifa NPS, AIG Hassan Aljir ameahidi kuwa maoni yaliyokusanywa katika kikao cha leo yatazingatiwa katika sera hiyo.
Sera mpya ya utendakazi wa maafisa wa akiba NPR itazingatia uongozi wa maafisa hao, uajiri, mafunzo pamoja na maslahi yao yanayojumuisha mishahara na sare kati ya masuala mengine.



Post Comment