Loading Now

Highlights

Viongozi wa Marsabit wametakiwa kuwapa wananchi misaada mbali mbali wakati huu wa kiangazi.

NA JB Nateleng

Wakazi wa Hurri hills wanakila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea malori mawili ya maji kutoka kwa mhisani mmoja.

Akizungumza na idhaa hii, Abudho Rahamata ambaye ni mkaazi wa eneo hilo amesema kwamba wamepokea maji hayo ambayo yatawasaidia katika kupambana na ukame ambayo imefanya bwawa na silanga kukauka katika eneo hilo jambo ambalo amesema inaendelea kuathiri wakazi.

Abudho amesema kwamba usaidizi huo ambao umetoka kwa mhisani Joyce Baye utawafaidi pakubwa kwani watapata maji ya kutumia kwa majukumu ya nyumbani pamoja na kuwapa mifugo huku akitoa wito zaidi kwa wahisani kuweza kuwasaidia.

Joyce Baye ambaye ni mmoja wa wanaowania kiti cha mwakilishi wa wanawake Marsabit mwaka wa 2027, amesema kwamba ametoa magari matatu ya maji ambayo mawili yashafika katika eneo la Huri hills huku gari moja likitarajiwa kufika katika eneo la Bori.

Joyce amewataka viongozi kusikilia kilio cha wananchi wa Marsabit na kuipa suluhu inayofaa haswa msimu huu wa kiangazi.

Ametoa wito wa ushirikiano baina ya viongozi waliopo serekalini, wanasiasa pamoja na watu wenye nia njema ili kuwasaidia wakazi wa Marsabit ambao wanakumbana na changamoto si haba.

Post Comment