Mwakilishi wa kina mama Naomi Waqo atoa wito kwa serikali kutoa chakula cha msaada kwa wakazi wa kaunti hii.
NYABANDE ORWA
Mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Marsabit, Naomi Jilo Waqo, ametoa wito kwa serikali kuongeza juhudi za kuwasaidia wakazi wa kaunti hiyo kwa chakula cha msaada wakati huu wa kiangazi.
Akizungumza wakati wa tamasha la kitamaduni la Tokummalililofanyika katika eneo la Dub Gobba, wadi ya Sagante Jaldesa, Naomi amesema watoto wanaoendelea na masomo ndio wanaoathirika zaidi na baa la njaa, kwa kuwa wengi wao hutegemea chakula cha shule ili kuweza kusoma na kustahimili njaa nyumbani.
Mwakilishi huyo amesema kuwa kama ilivyo kwa kaunti nyingine zinazokumbwa na njaa, Kaunti ya Marsabit inafaa kupewa kipaumbele katika ugawaji wa chakula cha msaada.
Kwa upande wake, Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, amesema serikali ya Rais William Ruto ina akiba ya kutosha ya chakula. Hata hivyo, amewataka viongozi katika ngazi mbalimbali kutoa taarifa mapema ili serikali iweze kuwafikia wananchi wanaohitaji msaada zaidi.
Katika hafla hiyo, serikali iligawa magunia 600 ya maharagwenamagunia 600 ya mchele kwa wakazi wa eneo la Dub Gobba.
Kuhusu ajira kwa vijana wa Kaunti ya Marsabit, Naomi amemtaka Waziri Ruku kuhakikisha vijana waliomaliza masomo wanapewa nafasi za ajira serikalini.



Post Comment