Loading Now

Highlights

Baadhi ya maeneo kaunti ya Marsabit kuendelea kupokea mvua katika kipindi cha siku saba zijazo

Na Caroline Waforo

Utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit katika siku 7 zijazo kuanzia leo tarehe 31 Machi hadi tarehe 6 Aprili, unaashiria uwepo wa mvua katika maeneo mbalimbali jimboni.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa kaunti ya Marsabit John Nguyo, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha nyakati za asubuhi, mchana na mvua zitakazoambatana na ngurumo nyakati za usiku.

Maeneo yatakayopokea mvua ni baadhi ya meneo Saku, Uran, Obbu, Butiye, Golbo, Dukana, Maikona na Illeret.

Aidha baadhi ya maeneo jimboni yatashuhudia upepo unaokwenda kwa kasi ya mita 12.9 kwa sekunde huku eneo la loingalani likitarajiwa kushuhudia upepo mkali

Hayo yakijiri wakaazi jimboni wameendelea kuhimizwa kuchukua tahadhari na kuepuka maeneo hatarishi huku mvua zikiendelea kunyesha.

Akizungumza na Shajara Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amewataka wanaoishi katika mikondo ya maji kuondoka ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.

Vile vile amewatahadharisha madereva akiwataka kuwa waangalifu barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika hasa msimu huu wa mvua.

Post Comment