Loading Now

Highlights

Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga azuru Saku, awahimiza wakaazi kujisajili kama wapiga kura

NA JB Nateleng

Mwaniaji wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kupitia chama cha UGM David Maraga, amewahimiza wakaazi wa Marsabit kujisajili kama wapiga kura ili kutekeleza haki yao ya kidemokrasia katika uchaguzi huo.

Akizungumza alipozuru eneo la Saku leo Alhamisi, Maraga amesema kwamba ni wakati sahihi kwa wananchi kuchagua viongozi bora akibainisha kuwa rasilimali zilizopo nchini zinatosha kukidhi mahitaji ya wakenya wote.

Vilevile Maraga amekosoa mradi wa serikali wa fedha za mtaji wa NYOTA akisema kuwa fedha hizo ni mkopo kutoka benki ya dunia.

Pia Maraga alitumia fursa hiyo kujipigia debe akiahidi kupambana na ufisadi nchini.

Wakati huo uo, baadhi ya wakazi wa Saku wametaja kutelekezwa na viongozi wao wakisisitiza kuwa ni wakati sahihi wa kuchagua kiongozi kwa vigezo vya maendeleo.

Post Comment