Wizara ya afya Marsabit yaanzisha uchunguzi wa mafua Laisamis.
Na Nyabande Orwa
Mkuu wa idara ya afya katika kaunti ndogo ya Laisamis, Yusuf Galmogle, amesema kuwa wameanza uchunguzi kuhusu ugonjwa wa mafua unaodaiwa kusambaa katika eneo hilo.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Galmogle amesema maafisa wa afya tayari wako mashinani wakichukua sampuli kutoka kwa wagonjwa ili zifanyiwe vipimo katika maabara ya KEMRI.
Amewahimiza wakazi wanaohisi dalili za mafua kufika katika vituo vya afya vilivyo karibu nao kwa uchunguzi na matibabu, wakati uchunguzi ukiendelea.
Wiki iliyopita, mwakilishi wa wadi ya Loiyangalani, Musa Emojo, aliitaka idara ya afya ya kaunti ya Marsabit kufanya uchunguzi wa haraka kubaini chanzo cha ongezeko la mafua katika eneo la Loiyangalani na maeneo ya jirani.
Kiongozi huyo alisema kuwa wakazi wengi, hasa watoto, wanaugua mafua na kikohozi kikali kwa wakati mmoja, hali ambayo si ya kawaida.



Post Comment