Loading Now

Highlights

Wandani wa Ukur Yattani wapinga UPIA kuhusishwa na upinzani.

Na Nyabande Orwa

Mwakilishi wa wadi ya Karare katika kaunti ya Marsabit, Joseph Leruk, amepinga madai kuwa kinara wa chama cha United Party of Independent Alliance (UPIA), Ukur Yattani, amejiunga na upinzani au kukiasi serikali ya Kenya Kwanza.

Akizungumza na kituo hiki, Leruk amesema chama cha UPIA bado kimesimama imara nyuma ya serikali ya Kenya Kwanza, licha ya baadhi ya viongozi waliokuwa awali katika muungano wa Azimio kuhamia upinzani.

Leruk amesema UPIA kinanuia kuwania viti vyote vya kisiasa katika kaunti ya Marsabit, isipokuwa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kauli yake inakuja takriban mwezi mmoja baada ya Ukur Yattani kuonekana katika mkutano wa viongozi wa upinzani uliohudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo Fred Matiang’i, Martha Karua naPeter Munya.

Wakati huo huo, Leruk ameunga mkono pendekezo la kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, linalowataka viongozi waliochaguliwa kutoka maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi kubaki mashinani katika kaunti zao ili kuimarisha utoaji wa huduma za kimsingi kwa wananchi.

Amesema badala ya viongozi kuwekeza rasilimali nyingi jijini Nairobi, ni vyema kuzingatia maendeleo ya miundombinu na huduma muhimu kwa wananchi waliowachagua.

Post Comment