Loading Now

Highlights

Wakazi wa Marsabit watahadharishwa kuhusu saratani ya njia ya uzazi

Na JB Nateleng

Mtaalam wa ugonjwa wa saratani katika hospitali ya rufaa ya MarsabitJoyce Mukoro, amewataka wakazi wa kaunti hii kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya HPV, ambavyo ni chanzo kikuu cha saratani ya njia ya uzazi.

Akizungumza na idhaa hii, Mukoro amesema njia pekee ya kubaini kama mtu ana virusi vya HPV ni kupitia vipimo hospitalini.

Ameeleza kwamba idara ya afya imebuni kifaa cha kibinafsi cha upimaji kinachomruhusu mtu kuchukua sampuli yake mwenyewe na kuipeleka kwa daktari kwa uchunguzi.

Mukoro amewaonya wazazi dhidi ya kuwapeleka wasichana katika zahanati au hospitali jirani ili wapate chanjo ya HPV.

Amesisitiza pia kuwa saratani ya njia ya uzazi ikiwa itagunduliwa mapema, mtu ana nafasi kubwa ya kupata tiba bora ikilinganishwa na kugunduliwa  kuchelewa.

Post Comment