Highlights

Visa vya utapiamlo vinaongezeka Marsabit.

Na Nyabande Orwa

Mkurugenzi wa Idara ya afya ya uzazi kaunti ya Marsabit, Bokayo Arero, amesema idadi ya visa vya utapiamlo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana.

Bokayo amesema asilimia 15 ya watoto wameathirika na utapiamlo, jambo lililosababishwa na ukame, umasikini, na kuondolewa kwa ufadhili wa lishe maalum kwa watoto walioathirika.

Ameongeza kuwa vituo vya afya sasa vinakabiliwa na idadi kubwa ya watoto waliyoathirika na utapiamlo.

Bokayo amesema wanashirikiana na sekta ya afya na wadau wengine kushughulikia ongezeko la visa vya utapiamlo.

Pia amewaonya kina mama kuweka usafi wa hali ya juu na kutafuta huduma za matibabu hospitalini, huku serikali ikitoa msaada wa chakula kwa watoto walioathirika zaidi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment