Highlights

Gavana Mohamud aahidi kushirikiana na vijana na kuongeza ajira Marsabit

Na JB Nateleng

Gavana wa Marsabit, Mohamud Ali, amekosoa wale wanaodai kuwa serikali yake haishughulikii masuala ya vijana.

Akizungumza alipofungua rasmi kongamano la vijana leo, Mohamud amesema serikali ya kaunti imetoa nafasi za ajira kwa vijana na kuhakikisha wanapata mazingira salama na mazuri ya kufanya kazi.

Gavana amesema hakuna kaunti nyingine nchini iliyo fanikiwa kama Marsabit katika kutoa nafasi za ajira kwa vijana.

Ameahidi kushirikiana na vijana katika masuala yanayowahusu na kuwajumuisha katika uongozi, akisema kwamba vijana ndio nguzo muhimu ya jamii imara.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment