Wakaazi wa Marsabit waunga mkono matamshi ya Gachagua, wataka uwajibikaji kutoka kwa viongozi
NA Joseph Muchai
Matamshi ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua aliyetuhumu viongozi wa maeneo ya Kaskazini mwa nchi kwa kushindwa kufanikisha maendeleo licha ya kupokea mgao mkubwa wa kifedha kutoka serikali kuu yameungwa mkono na baadhi ya wananchi kutoka mjini Marsabit.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani wakaazi hao wamesema kuwa viongozi wao wamezembea katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
CUE IN…WAKAAZI ON GACHAGUA
Aidha, wakaazi hao wameeleza kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwekeza katika kaunti nyingine, huku wakiyaacha maeneo yao yakikumbwa na changamoto sugu kama ukosefu wa elimu bora.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Marsabit human right defenders Mohamed Hassan, amedai kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakifuja fedha za umma zilizotengewa maendeleo
Hassan ameihimiza serikali ya kitaifa kutoshirikiana na viongozi wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi, huku akimtaka rais William Ruto kupambana na ufisadi alivyoahidi wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Kauli hizi zinajiri siku chache baada ya kinara wa DCP Rigathi Gachagua kudai kuwa mfumo wa kuwachagulia shule wanafunzi wanaojiunga na shule za upili ulikuwa na ubaguzi ambapo wanafunzi kutoka maeneo ya mlimani walikosa nafasi kwenye shule zilizoko Mlimani kutokana nafasi zao kuchukuliwa na wanafunzi kutoka maeneo mengine kama vile kaskazini mwa nchi.
Alihusisha tatizo hilo na uhaba wa shule maeneo ya Kaskazini tatizo linalotokana na kuzembea kwa viongozi wa maeneo hayo.



Post Comment