Loading Now

Highlights

Wafugaji Marsabit wahimizwa kutafuta usaidizi wa kitabibu wanapokabiliwa na changamoto za afya ya akili

NA Caroline Waforo

Wafugaji katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutafuta huduma za afya ya akili hasa msimu huu ambapo wengi wao wanaendelea kukabiliana na athari za kiangazi.

Kulingana na mtaalam wa afya ya akili katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Marsabit Dr Victor Karani, athari za kiangazi zinaweza kusababisha msongo wa mawazo miongoni mwa wafugaji wanaotegemea mifugo kama chanzo kikuu cha riziki yao.

Hii ni kutokana na hali kwamba wakati wa msimu wa kiangazi kuna upungufu wa maji na lishe kwa mifugo na hivyo kupelekea kudhoofika kwa afya ya mifugo hao.

Post Comment