Loading Now

Highlights

Upatikanaji wa dawa za kulevya kwa urahisi wachochea matumizi miongoni mwa wanafunzi Marsabit

NA Caroline Waforo

Upatikanaji wa dawa za kulevya kwa urahisi, ugumu wa maisha pamoja na changamoto za afya ya akili ni miongoni mwa sababu zinazochochea matumuzi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi katika kaunti ya Marsabit.

Akizungumza katika chuo cha KMTC tawi la Marsabit wakati wa kilele cha kampeni ya siku tano ya kutoa hamasa dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, Mratibu wa Mamlaka ya NACADA tawi la Marsabit Mohammed Wako, amesema kuwa baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali wamedai kupata dawa hizo kupitia baadhi ya waendesha bodaboda wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Vilevile amesisitiza haja ya kundelea kuhamasisha wanafunzi na vijana kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu huku akiwahimiza wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao mazingira bora nyumbani ili kuwakinga dhidi ya kujihusisha na matumizi hayo.

Kadhalika Wako amedokeza kuwa mamlaka hiyo ya NACADA Marsabit, imeanza kutoa huduma za ushauri nasaha kwa wanafunzi wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili.

Leo Ijumaa mamlaka ya NACADA imekamilisha kampeni ya siku tano ya kuhamasisha umma dhidi ya matumizi dawa za kulevya na pombe haramu.

Kampeni hiyo imelenga makundi mbalimabli ikiwemo vijana, wafanyibiashara wa vileo pamoja na akina mama wanaodaiwa kujihusisha katika uuzaji wa pombe haramu na ambao wamewezeshwa ili kujihusisha na shughuli mbadala za kujitafutia mapato.

Post Comment