Ukeketaji imetajwa kuwa mojawapo ya sababu ya ugonjwa wa fistula Marsabit.
Na Samuel Kosgei
2223
Akizungumza katika hafla ya kujadili mbinu za kukabiliana na dhuluma za kijinsia na kuhamasisha haki za mtoto msichana, Bokayo amesema kuwa ukeketaji (FGM) kwa kiasi kikubwa huchangia tatizo la wanawake kushindwa kuzuia mkojo au haja kubwa, hali inayojulikana kama fistula.
Suala lingine kuu linalochangia shida hiyo ni wasichana kuolewa wangali wadogo na wanapojifungua hupitia hali ngumu kwani viungo vya mwili bado havijakomaa.
Amewahimiza wanawake waliohudhuria kikao hicho kusaidia kueneza ujumbe wa kupinga na kutokomeza ukeketaji wa wasichana, akisisitiza kuwa mila hiyo ni kinyume na haki za binadamu na inaleta madhara makubwa kiafya.
Wito wake unajiri siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake jana, Jumapili.



Post Comment