Saratani ya umio yawaathiri wengi Marsabit.
NA Sabalua Moses
Saratani ya umio ni miongoni mwa saratani zinazoongoza katika kaunti ya Marsabit.
Kwa mujibu wa muuguzi anayesimamia matibabu ya saratani katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Marsabit, Joyce Mukuro, ugonjwa huo unaathiri wakaazi wengi wa kaunti hiyo.
Akizungumza na kituo hiki, Mukuro amehimiza wakaazi kutembelea hospitali mapema kwa uchunguzi na matibabu, na kuacha kutumia miti shamba kama tiba mbadala ya saratani.
Aidha amesema changamoto kubwa ni kuishawishi jamii kuwa na imani na hospitali, akieleza kuwa baadhi ya wagonjwa hutumia miti shamba ambayo mara nyingi huharibu figo na viungo vingine vya mwili.
Hata hivyo, Joyce amewataka wakaazi hususan kutoka jamii za wafugaji kujenga utamaduni wa kutembelea hospitali mara kwa mara kwa ajili ya vipimo. Amesema kufanya hivyo kutasaidia kugundua saratani mapema na kupata matibabu kwa wakati.



Post Comment