Loading Now

Highlights

Muungano wa walimu wakuu Marsabit (KESSHA) wataka Elimu Ipewe Kipaumbele Miongoni mwa Jamii za Wafugaji

Na Samuel Kosgei

Mwenyekiti wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili (KESSHA) kaunti ya Marsabit, Halima Adan, amewataka wazazi kutoka jamii za wafugaji kuwapeleka watoto wao shuleni badala ya kuwaruhusu kulisha mifugo.

Akizungumza katika hafla ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Upili ya Merile, Halima amesema inasikitisha kuona watoto wakilisha mifugo kando ya barabara kuu ya Marsabit–Isiolo badala ya kuwa darasani wakipata elimu. Ameeleza kuwa elimu ndiyo msingi wa maisha bora ya baadaye na njia ya kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi.

Wito huo umeungwa mkono na Naibu Chifu wa Merile, Evans Letapo, ambaye amesisitiza umuhimu wa wazazi kuachana na mila na desturi zinazowazuia watoto kuhudhuria masomo.

Amewahimiza wazazi kuipa elimu kipaumbele na kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kuchunga mifugo badala ya kuwapeleka shuleni.

Letapo amesema miundombinu ya Shule ya Upili ya Merile kwa sasa iko katika hali nzuri na inatosheleza mahitaji ya wanafunzi, hivyo hakuna sababu ya watoto kukosa masomo.

Post Comment