Loading Now

Highlights

Mca Leruk ataka serikali kuu ichukue usimamizi wa barabara ya Badasa–Karare

Na Nyabande Orwa

Mwakilishi wa wadi ya Karare, Joseph Leruk, ametoa wito kwa serikali kuu kuchukua usimamizi wa ukarabati wa barabara ya Badasa–Songa hadi Karare.

Kwa mujibu wa Leruk, barabara hiyo ni muhimu sana kwa masuala ya usalama na mipango ya kimkakati katika kaunti ya Marsabit. Amesema uzito wa barabara hiyo unaifanya iwe vigumu kwa serikali ya kaunti kuitengea fedha za kutosha kwa ajili ya ukarabati na kuifikisha katika kiwango kinachohitajika.

Kiongozi huyo amedai kuwa Naibu Rais, Profesa Kithure Kindiki, alipokuwa waziri wa usalama wa ndani, pamoja na waziri wa sasa Kipchumba Murkomen, waliwahi kutembelea barabara hiyo, wakaona umuhimu wake na kuahidi kuingilia kati ili ikarabatiwe. Hata hivyo, hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

Leruk hata hivyo amesema kuna matumaini, akieleza kuwa kupitia mfuko wa ushuru wa mafuta, barabara hiyo sasa imetengewa bajeti ya kufanyiwa ukarabati.

Post Comment