Mamlaka ya NDMA yatangaza hali ya ukame na onyo la mapema katika Kaunti ya Marsabit.
NA Samuel Kosgei
Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Ukame, NDMA, katika Kaunti ya Marsabit imetoa onyo la mapema kuhusu kuendelea kudorora kwa hali ya ukame.
NDMA inasema kaunti ilipokea asilimia 63 pekee ya mvua za kawaida za msimu wa mvua fupi Oct- Nov na December OND, hali iliyosababisha kupungua kwa uwezo wa malisho na mimeo na pia kukauka kwa vyanzo vya maji. Visima virefu pia vinaripotiwa kuharibika mara kwa mara.
Hali ya mifugo kwa sasa ni ya wastani hadi nzuri, hata hivyo uzalishaji wa maziwa umepungua huku magonjwa ya mifugo yakiongezeka katika maeneo ya Moyale, Laisamis, North Horr na Saku.
Aidha, upatikanaji wa maji umeendelea kuwa changamoto kubwa, ambapo familia na mifugo wanalazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.
NDMA imewataka wadau na jamii kuchukua tahadhari mapema ili kupunguza athari za ukame unaoendelea katika kaunti ya Marsabit.



Post Comment