Loading Now

Highlights

Kanisa Katoliki lawataka vijana kutumia teknolojia kueneza injili

Na JB Nateleng

Kanisa Katoliki limetoa wito kwa vijana kutumia teknolojia kwa njia inayochangia ukuaji wa kiroho, maendeleo ya kijamii na kuheshimu hadhi ya binadamu.

Haya yamebainishwa katika tafakari ya wiki ya nne ya Kwaresma, inayozingatia maslahi ya vijana pamoja na matumizi ya teknolojia.

Kwa mujibu wa kanisa, vijana wengi katika karne hii hutumia sana majukwaa kama vile TikTok, Instagram, WhatsApp, Facebook na YouTube kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo kujifunza, kujitafutia mapato pamoja na kufuatilia ibada.

Hata hivyo Kanisa limeonya licha ya hayo kuna hatari na changamoto zinazoweza kujitokeza hasa kutokana na shinikizo la kutafuta pesa na ukosefu wa kina kuhusu matumizi sahihi ya mifumo na majukwaa ya kidijitali.

Wakati huo huo Baba Mtakatifu Francis pamoja na mrithi wake, Papa Leo XIV, wametoa mwongozo muhimu kuhusu matumizi ya akili mnemba (AI), wakisisitiza umuhimu wa utaratibu unaomjali binadamu.

Kanisa pia limehimiza ushirikiano kati ya serikali, kijamii, Kanisa na watetezi wa haki ili kuhakikisha matumizi ya majukwaa ya kidijitali yanaheshimu hadhi ya binadamu, kulinda haki za kiuchumi na kuchangia katika ukuaji wa kiroho huku yakizuia matumizi mabaya ya data za wananchi.

Post Comment