Highlights

Idara ya usalama Marsabit yasema inachunguza mauaji ya hivi maajuzi katika migodi ya Hillo

Na Caroline Waforo

Idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit imesema kuwa inaendelea na uchunguzi wa mauaji ya hivi maajuzi katika migodi ya Hillo iliyoko lokesheni ya Dabel, kufuatia mzozo baina ya jamii mbili.

Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema kuwa uchunguzi huo unawalenga wahusika pamoja na watu wanaodaiwa kuchochea mzozo huo.

Kamishna Kamau ametoa onyo kwa watu walio na silaha haramu katika migodi hiyo iliyopigwa marufuku kutokana na sababu za kiusalama, akisema kuwa watakamatwa na kuwajibishwa kisheria.

Vilevile amezitaka jamii hizo mbili kutoa taarifa muhimu kufanikisha uchunguzi huku akizitaka kudumisha amani.

Haya yanajiri wakati ambapo gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali ameendelea kuitaka idara hiyo ya usalama kuhakikisha kuwa waliotekeleza mauaji hayo wamekamatwa na kuwajibishwa huku akiituhumu idara hiyo kwa kile anadai ni kuhangaisha raia wasiokuwa na hatia.

Post Comment