Loading Now

Highlights

Wazazi Marsabit watakiwa kufuatilia watoto wakati wa likizo fupi

NA JB Nateleng

Huku wanafunzi wakiwa nyumbani kwa likizo fupi ya muhula wa kwanza wito, umetolewa kwa wazazi kufuatilia tabia za watoto wao ili kuwazuia kujiingiza katika makundi haramu.

Akizungumza katika jukwaa la vijana, kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema wanafunzi wengi msimu huu ndio wanajiingiza katika makundi ya matumizi ya dawa za kulevya na uhuni.

Kamau pia amesema ni wajibu wa kila mzazi kumakinika na miendendo ya mtoto wake kwa manufaa ya jamii bora.

Aidha ametetea mradi wa mgao wa NYOTA ambao amesema kwamba ni wa manufaa sana huku akiwarai vijana waliopata fedha hizo katika kaunti ya Marsabit kuzitumia kwa njia sahihi ili kujikuza kiuchumi.

Post Comment