Loading Now

Highlights

Washikadau mjini Marsabit watetea nafasi ya mtoto wa kiume katika jamii.

NA NYABANDE ORWA

Wakati mashirika mbalimbali na wadau wakielekeza juhudi zao kwa mtoto wa kike, mtoto wa kiume anaonekana kusahaulika. Kauli hii imetolewa na Christopher Galgalo, ambaye ni msomi na mtetezi wa masuala ya elimu.

Akizungumza na wanahabari, Galgalo amesema kuwa katika jamii nyingi za Kaskazini mwa nchi, mtoto wa kiume ameendelea kutelekezwa kielimu na kubaki kutekeleza mila na majukumu ya kijamii kama kuchunga mifugo. Ameeleza kuwa hali hii imesababisha mtoto wa kike kuwezeshwa zaidi, huku mtoto wa kiume akiachwa nyuma.

Kauli hii inaungwa mkono na Afisa wa Watoto katika kaunti ya Marsabit, Leakey Mukanzi, ambaye amesema kuwa serikali imekuwa ikihamasisha jamii za wafugaji kuwapeleka watoto wao shule. Hata hivyo, amesema juhudi hizo zinaendelea kuzaa matunda kwa mwendo wa polepole kutokana na mila na tamaduni zilizokita mizizi katika jamii hizo.

Kwa mujibu wa Galgalo, ili kuleta usawa wa kijinsia, ni muhimu watoto wa kike na wa kiume kupewa fursa sawa ya elimu na kuelekezwa kuhusu umuhimu wa taaluma, badala ya kubagua jinsia moja.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Marsabit, Simon Arome, amesema idara ya mahakama inaendelea kuhakikisha haki za mtoto wa kiume zinalindwa kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Kenya. Amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wa kiume kuhudhuria masomo badala ya kuwaacha wakijishughulisha na kuchunga mifugo pekee.

Cue in Arome on boy child

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment