Loading Now

Highlights

Wanaoendeleza ukeketaji Marsabit waonywa

NA JAMES MUCHAI

Watu wanaoendeleza ukeketaji katika kaunti ya Marsabit wameonywa vikali dhidi ya kuendelea kutekeleza tamaduni hiyo iliyopitwa na wakati.

Akizungumza na wanahabari habari mjini Marsabit, Naibu mwenyekiti wa amani katika kaunti hii, Adan Chukulisa, amesema kuwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na kitendo hicho atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, Chukulisa amewataka wazazi kuwachunga na kuwalinda watoto wao msimu huu wa likizo ndefu, huku akionya kuhusu hatari ya dawa za kulevya. Ameeleza kuwa walimu wametekeleza jukumu lao wakati wa muhula wa masomo, na sasa ni wajibu wa wazazi kuhakikisha usalama na malezi bora ya watoto wao.

Amesisitiza pia umuhimu wa vijana kujiepusha na dawa za kulevya, uhalifu na uhasama, akiwashauri kujihusisha na masuala ya michezo ili kujijenga kimwili na kiakili.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment