Ushirikiano wa Wananchi Watakiwa Kukomesha Wizi wa Mifugo Laisamis.
Na Samuel Kosgei
Wakazi wa kaunti ndogo ya Laisamis wametakiwa kushirikiana na maafisa wa polisi kwenye mapambano dhidi ya wizi wa mifugo.
Akizungumza na kituo hiki, Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Laisamis, Mohamed Mwakio, amewahimiza hasa wasimamizi wa masoko ya mifugo kuwa makini na kuhakikisha mifugo wanayonunua au kuruhusu kuuzwa ina asili halali. Amesema ununuzi wa mifugo ya wizi ni sawa na kuwasaidia wahalifu kuendeleza uhalifu wao.
Onyo hilo linajiri siku chache baada ya ngamia aliyeripotiwa kuibwa katika eneo la Shurr kupatikana katika soko la mifugo la Merile, tukio lililosababisha mvutano kati ya polisi na baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo.Wakazi wa kaunti ndogo ya Laisamis wametakiwa kushirikiana na maafisa wa polisi kwenye mapambano dhidi ya wizi wa mifugo.
Akizungumza na kituo hiki, Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Laisamis, Mohamed Mwakio, amewahimiza hasa wasimamizi wa masoko ya mifugo kuwa makini na kuhakikisha mifugo wanayonunua au kuruhusu kuuzwa ina asili halali. Amesema ununuzi wa mifugo ya wizi ni sawa na kuwasaidia wahalifu kuendeleza uhalifu wao.
Onyo hilo linajiri siku chache baada ya ngamia aliyeripotiwa kuibwa katika eneo la Shurr kupatikana katika soko la mifugo la Merile, tukio lililosababisha mvutano kati ya polisi na baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo.

Post Comment