Wakaazi wa kaunti ya Marsabit waombwa kujitolea katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
NA Joseph Muchai
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kujitolea kikamilifu katika kupambana na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Akizungumza na Radio Jangwani, mwanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya kaunti ya Marsabit, Fredrick Ochieng, amesema kuwa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwaficha wauzaji wa dawa hizo hatari.
Amesema hatua hiyo inachangiwa na hofu na kile wanachokiita maonevu dhidi ya jamii zao.
Ochieng amesema tabia hiyo imeendelea kuharibu maisha na mustakabali wa vijana wengi, wakiwemo watoto na ndugu wa karibu wa wananchi wenyewe.
Ameongeza kuwa mara nyingi wanajamii hushindwa kutekeleza wajibu wao wa kupambana na dawa za kulevya, kisha huishia kulaumu serikali na wadau wengine kwa kile wanachodai ni uzembe.
Wakati huohuo, Ochieng amepongeza juhudi za Rais William Ruto katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Hata hivyo, amelalamikia baadhi ya baa kufunguliwa mapema kabla ya muda unaoruhusiwa kisheria, hali anayosema inaweka maisha ya wengi hatarini.
JaimeGah
this article



1 comment