Loading Now

Highlights

Viongozi wa kisiasa watakiwa kuhubiri amani Marsabit

NA Sabalua Moses

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhubiri amani hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027, ili kuepusha migawanyiko miongoni mwa wanajamii.

Akizungumza na Shajara, Kasisi Joseph Mwendwa kutoka kanisa la Kenya Assemblies of God mjini Marsabit, amesema kuwa viongozi wana wajibu wa kuhubiri amani na kujiepusha na matamshi yanayoweza kuzua chuki au migawinyiko.

Aidha Kasisi Mwendwa amewataka wanasiasa kuwa waangalifu na matamshi yao wanapoanza siasa za mapema, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana, kutodhalilishana na kuheshimu usawa wa kijinsia katika siasa.

Post Comment