Loading Now

Highlights

Viongozi wa kidini Marsabit wahimizwa kuunga mkono vita dhidi ya ukeketaji.

NA JB Nateleng

Kama njia ya kuimarisha vita dhidi ya ukeketaji katika kaunti ya Marsabit, shirika la kutetea haki za wanawake MWADO, limeandaa warsha ya kuwaelimisha viongozi wa dini la Kiislamu kuhusu umuhimu wa kulinda haki za watoto wa kike.

Mkutano huo umewaleta pamoja Maimamu na Masheikh kutoka misikiti mbalimbali ya Marsabit, ambapo wamepokea mafunzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Dini ya Kiislamu (CIPK) tawi la Tana River Sheikh Abdullahi Hajji.

Sheikh Hajji amewahimiza viongozi hao wa kidini kuwa katika mstari wa mbele katika kupinga ukeketaji wa wasichana.

Vilevile Sheikh Hajji amesisitiza kwamba dini haiungi mkono ukeketaji, akiwataka walezi kuwalinda watoto wa kike dhidi ya tamaduni hiyo iliyopitwa na wakati.

Wakati uo huo mwasisi wa MWADO Nuria Gollo amewahimiza viongozi hao wa kidini kukumbatia mafunzo hayo na kuyatumia kuhamasisha jamii kukomesha ukeketaji.

Post Comment