Highlights

Maafisa wa Kliniki Marsabit kuendelea na mgomo wao.

NA Sabalua Moses

Mgomo wa maafisa wa kliniki KUCO tawi la Marsabit unaendelea licha ya muungano wa kitaifa kusitisha mgomo hapo jana.

Kulingana na katibu wa maafisa hao Daki Duba mgomo huo bado ungalipo kwani serikali ya kaunti imeshindwa kutekeleza matakwa yao.

Daki amesema kuwa kufikia sasa hajawalipwa mishahara ya miezi miwili huku maafisa hao wakihisi kudhalilishwa na serikali ya kaunti ya Marsabit.

Katika makubaliano yaliyotiwa saini hapo jana Jumatatu kati ya Muungano wa KUCO na magavana, kaunti 3 kati ya 47 zilikataa kusitisha mgomo huo.

Kaunti hizo ni pamoja na kaunti hii ya Marsabit, Baringo na kaunti ya Nairobi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment