Loading Now

Highlights

Vijana wahimizwa kukumbatia masomo ya Vyuo vya Anuwai

NA JB Nateleng

Wito umetolewa kwa vijana katika kaunti ya Marsabit kukumbatia masomo ya Vyuo vya Anuwai ili kupata ujuzi wa kujiajiri na kuwa wabunifu katika kutengeneza nafasi za ajira.

Kauli hii imetolewa na Msimamizi Mkuu wa chuo cha Anuwai cha Don Bosco Padri Sunil Orathel ambaye amesema kuwa vyuo vya anuwai vimeratibiwa kwa lengo la kuwapa vijana ujuzi unaoweza kubadilisha maisha ya vijana.

Padri Sunil ameelezea kwamba ni wakati mwafaka wa vijana waliomaliza kidato cha nne na wale ambao hawakufanikiwa kumaliza masomo ya shule ya upili kuanza mafunzo katika vyuo vya anuwai zinazopatikana jimboni.

Aidha, Padri Sunil ameeleza kuwa masomo katika vyuo vya anuwai huchukua muda mfupi, jambo linalowezesha vijana kupata ujuzi wa haraka.

Vile vile amewakosoa wale ambao wanadunisha masomo yanayopatikana katika Vyuo vya Anuwai akisisitiza kwamba vyuo hivi hutoa mafunzo bora na yenye ustadi wa hali ya juu.

Haya yanajiri wakati ambapo wengi wa watahiniwa waliofanya mtihani wa KCSE wa 2025 hawakufanikiwa kupata alama ya kuwapeleka vyuo vikuu moja kwa moja.

Ni watahiniwa 270,715 katia ya 993,226 walipata alama ya wastani ya C+ au zaidi, wakistahiki kuingia vyuo vikuu 

Post Comment